Taarifa kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye.

December 15 2016 Dr. Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya jana.

Taarifa kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye.

December 15 2016 Dr. Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya jana.

Wadau nipo nyumbani kwa takribani mwezi sasa baada ya kumaliza mkataba wangu na kampuni flani.sasa hapa nyumbani ninaishi na wife na kidi wangu wa miaka 3..na nimekuta wife kamleta mdogo wake wa kike ambaye amemaliza chuo mwaka jana anasubiria ajira,sasa wadau wife wangu ni mfanyakazi so mida mwingi anashinda job,mimi nipo tu home na shemeji yangu,kid anapelekwa shule asubuh mpska jioni.shem huyu wadau ni mrembo sana ana figure matata sana na ni mzuri kwa kweli..yani mitihani ninayoipata ni mikubwa sana..mana nguo anazo vaa zinaonenya umbo lake namba 8 lilivyo,juzi asubuh nilikuwa nimelala akagonga chumbani kwangu anatafuta kitu wakati kavaa khanga tu.jamani naombeni ushauri wenu nifanyaje je?maana uzalendo unaelekea kunishinda asee.maana sasa imefika wakati naliota umbo lake na uzuri wake nimechanganyikiwa.naombeni ushauri weni wadau.

Asanteni

By Fukara




ZARI DIAMOND (2)
Mwandishi wetu
Mastaa wawili wakubwa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wanadaiwa kuangusha bonge la pati yenye kila aina ya viashiria vya ufuska, Risasi Jumamosi limeinyaka.
ZARI DIAMOND (3)Pati hiyo ya aina yake ilifanyika ndani ya mjengo wa Diamond (white house) uliopo pande za Madale-Tegeta jijini Dar, usiku wa kuamkia siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj (Alhamis iliyopita) na kuhudhuriwa na watu maalum tu, ikiwa ni katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Zari.
Chanzo chetu cha kuaminika ambacho kilikuwa miongoni mwa waalikwa kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, siku hiyo ilikuwa ya kipekee kwa mastaa hao licha ya kwamba yaliyofanyika hayakuwa na sura nzuri mbele ya jamii.
ZARI DIAMOND (4)POMBE KWA SANA
Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, awali, waalikwa wakiwemo mastaa kadhaa walianza ‘kupiga maji’ kwa staili ya taratibu au mdogomdogo hali iliyowafanya kadiri muda ulivyokuwa ukisonga, ndivyo walivyokuwa ‘wakipendeza’.
“Ilikuwa pati ya kufuru lakini watu walikuwa wachache na maalum, waalikwa walianza kwa kupata vinywaji mbalimbali na wale ambao ni watumiaji wa ‘maji machungu’ nao walipata chansi ya kujisevia walichotaka.
“Kwa kuwa pombe zilikuwa za kumwaga, watu walipombeka sana na ulipoingia usiku mnene, wengi walikuwa chicha,” kilidai chanzo hicho.
ZARI DIAMOND (1)MUDA WA KUOGELEA
Ilidaiwa kuwa, wakati wengine wakiendelea kuburudika, baadhi walifikia hatua ya kusaula na kujirusha kwenye ‘swimming pool’ (bwawa la kuogelea) iliyopo nyumbani hapo na kuanza kuogelea na wakati mwingine kucheza muziki.
ZARI DIAMOND (6)“Kuna wakati baadhi ya watu walijitoa ufahamu kwa kusaula na kubaki na nguo za kuogelea kisha kuzama kwenye bwawa na kuanza kupiga mbizi.
“Si unajua tena watu walikuwa nusu uchi, halafu baadhi walikuwa bwii, sasa unaweza kuvuta picha kilichokuwa kikiendelea kwenye maji, hata hivyo, ilikuwa full burudani aiseee,” kilitiririka chanzo hicho.
ZARI DIAMOND (7)KWA NINI PATI YA UFUSKA?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mambo waliyokuwa wakifanya ndani ya mjengo huo hayakuwa ya kistaarabu kwani kubambiana ilikuwa sehemu ya shughuli hiyo.
ZARI DIAMOND (8)“Zari mwenyewe alikuwa ndani ya Swimming Costumes (nguo za kuogelea) na mawifi zake akina Esma na Queen Darleen, Diamond mwenyewe, Shetta na wengine ndani ya maji, wakajiachia kisawasawa huku watu wakiwatazama na muziki wa kufa mtu ukipigwa.
“Lakini wapo baadhi ya wanaume ambao hawakuwa wastaraabu kwani walifanya vitendo ambavyo havikuwa vya kistaarabu tena kwa wanawake ambao siyo wao, ilikuwa na sura f’lani ya ufuska.
ZARI DIAMOND (9)“Pia wapo baadhi ambao ni Waislam na usiku ule asubuhi yake ilikuwa Sikukuu ya Idd, sasa kufanya tukio lile kwa wakati ule, kusema kweli halikuwa jambo zuri kiimani hasa kwa familia kama ya Diamond,” kililalama chanzo hicho.
ZARI DIAMOND (11)ILIKUWA PATI YA SIRI
Chanzo hicho kiliendelea kunyetisha kwamba, pati hiyo iliyofanyika kwa siri huku mapaparazi wakinyimwa nafasi ya kushuhudia kilichokuwa kikiendelea ndani ya jumba la staa huyo ilihudhuriwa na baadhi ya mastaa wachache wakiwemo Shetta, Queen Darleen, TID, Young Dee, Romy Jones na wengine ambao walikuwa ni maalum.
ZARI DIAMOND (13)Habari zinaeleza kuwa, katika pati hiyo, Zari au mama Tiffah alikuwa akitimiza umri wa miaka 35 tangu alipoliona jua.


Kazi ipo mwaka huu! Ndugu wa mzazi mwenzake na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamempa zawadi mtoto wa mastaa hao, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ ndinga aina ya Mercedes Benz MSL Benz lenye thamani ya dola 100,000 (zaidi Sh. milioni 200).

Habari za uhakika kutoka ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba, ishu hiyo ilijiri juzikati mara tu baada ya Zari ambapo baadhi ya ndugu wa mwanamama huyo walichanga na kumletea Tiffah gari hilo ili Zari alitumie katika mishemishe zake anapotoka na mwanaye Tiffah ikiwa ni pamoja na kumpeleka kliniki.

Kikisherehesha kwa kina stori hiyo, chanzo hicho kiliweka bayana kuwa ndugu wa Tiffah wameamua kumletea gari hilo ikiwa ni moja ya zawadi ambazo waliahidi kipindi akiwa majamzito, lakini pia wameamua kufanya hivyo kwa kuwa hawataki mtu achangie gari na Tiffah.

“Ni kweli ndugu wa Zari wameamua kumnunulia Tiffah gari aina ya Benz na tayari limewasili Bongo na Ijumaa iliyopita lilitumika kumpeleka Tiffah kliniki,” kilisema Chanzo hicho cha ndani.




 Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha kukataliwa.

MINONG’ONO

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda harusi inayofuata itakuwa yao.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo haliwezekani huku sababu nne zikianikwa.

KIGEZO CHA DINI

Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho.

NDOA ZA MASTAA NI TATIZO?
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.

KIGEZO CHA KABILA

Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni M uha.

KIGEZO CHA BONGO FLEVA
Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini.

KAMA DIAMOND

“Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate.
“Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho.

KIBA KAMA KAWA

Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

TUJIKUMBUSHE

Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa jamaa huyo ni mtu wake.


CREDIT: GPL


Muda  huu  polisi  wanapiga mabomu  uwanja  wa  ndege   jijini  Mwanza kuwatawanya  wananchi  waliokusanyika  kumpokea  Lowassa.
Mabomu  yamepigwa  muda  mfupi  baada  ya  ndege  inayosadikiwa  kuwa  ni  ya  Lowassa  kutua  uwanjan, hali  iliyowafanya  wananchi  walipuke  kwa  furaha  huku  wakiimba  nyimbo  za  Chadema.
Kadhia  hiyo  iliwafanya  Polisi  watumie nguvu  ya  ziada  kuwatawanya  wananchi hao  waliokuwa  wametanda  barabarani.

“KWANGU mimi kuingia Ikulu ni tunda la lengo kuu ambalo ni kurudisha maadili ndani ya nchi hii. Nani hajaona matumizi ya rushwa kwenye mchakato wa Lowassa kutafuta wadhamini? Leo fedha zinazotumika ni za kina Rostam Aziz – wale wale ambao tukisimama jukwaani tumekuwa tukiwaita mafisadi. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu” (Dk. Slaa – Agosti 3, 2015).
“Nawaomba radhi sana wanachama na wananchi walioniamini na kuonyesha mapenzi makubwa kwangu na uongozi wangu. Nimeshiriki vikao vya Ukawa vilivyotufikisha hapa. Hata hivyo, dhamira na nafsi yangu inanisuta kuwa katika uamuzi wetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia tunu za Taifa za utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji” (Profesa Lipumba – Agosti 6, 2015).

Ndugu zangu, nimeshawishika kuanza na nukuu hizo mbili za waliokuwa vigogo wa Ukawa walioachia nyadhifa zao hivi karibuni kwa kusutwa na dhamira zao juu ya ujio wa Edward Lowassa katika umoja huo. Namaanisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba.

Wote wawili wameziachia nyadhifa zao walizozishika kwa miaka mingi kwa sababu ya kusutwa na dhamira zao baada ya Ukawa kumpokea Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais wao kupitia Chadema. Ni hatua ambazo zinathibitisha busara zao, ukomavu wao kisiasa, weledi, uadilifu na heshima zao kwa umma.

Daima nitawaheshimu watu ambao hupoteza karibu ‘kila kitu’ kwa kujiuzulu nyadhifa zao za uongozi kwa sababu tu ya kusutwa na dhamira zao. Si siri kwamba dunia ina watu wachache wenye ujasiri huo wa kutii na kuheshimu dhamira zao.

Katika andiko lake – A Testament of Hope, mpigania haki za watu weusi wa zamani wa Marekani, Martin Luther King Jr. anasema hivi: “There comes a time when one must take a position that is neither safe nor popular but he must take it because conscience tells him it is right (kuna wakati ambapo mtu huchukua hatua au msimamo ambao si salama wala unaopendwa lakini ni lazima auchukue kwa kuwa dhamira inamwelekeza ya kuwa ni kitu sahihi kukifanya).

Kwa mantiki hiyo, nawapongeza Dk. Slaa na Profesa Lipumba kwa kuketi chini, kutafakari na kusemezana na nafsi zao, na kisha kufikia hatua ya kujiuzulu nyadhifa zao kuliko kuendelea na Ukawa ya Edward Lowassa. Wasingefanya hivyo, dhamira zingeendelea kuwasuta maisha yao yote kwa sababu walishiriki kueneza imani nchini kuwa ni fisadi. Nawapongeza kwa kuzishinda roho za kinafiki na za ubinafsi zilizojaa uchu wa pesa na madaraka.

Kwa hiyo, historia itakuja kuandikwa ya kwamba Dk. Slaa na Profesa Lipumba waliachia nyadhifa zao baada ya dhamira kuwasuta kwa kushiriki mchakato wa kumkaribisha Lowassa katika Ukawa, na hata kumfanya mgombea urais wao. Yaani Lowassa yule yule ambaye kwa miaka kadhaa walikuwa wakimpigia kelele nchi nzima kuwa ni fisadi! Yaani Lowassa yule yule aliyeibariki na kuipigia kura ya NDIYO Katiba Pendekezwa inayopingwa na Ukawa!

Ndiyo maana katika kutafakari hatua yao hiyo ya kijasiri, nimesononeshwa na lugha aliyoitumia kijana John Mnyika wa Chadema katika kumkosoa Profesa Lipumba kwa kuchukua hatua aliyoichukua. Mnyika ni kijana mdogo mno kwa Profesa Lipumba. Mnyika hamkaribii kisiasa, kielimu wala kiumri Profesa Lipumba, na hivyo alipaswa kumkosoa kiungwana.

Namshauri amsome mwanafalsafa wa zamani wa Ufaransa, Jean-Jacques Rousseau katika andiko lake kuhusu asili ya kupotea kwa usawa duniani (Origins of Inequality – page 81 part two). Rousseau anasema hivi: “Contrary to the law of nature however it may be defined, for a child to command an old man, for an imbecile to lead a wise man, and for a handful of people to gorge themselves on superfluities while the starving multitudes lacks necessities.”

Kwa ufupi anashomaanisha Rousseau, miongoni mwa mambo mengine, ni kwamba ni kinyume cha sheria ya asili kwa mdogo kumfokea au kumwamrisha mkubwa. Kosa hilo ni sawa na lile la mjinga kumwongoza mwerevu. Naamini Mnyika ananielewa, na kama ananielewa, basi naye iko siku dhamira itamsuta na kumwomba radhi Profesa Lipumba!

Hayo pembeni, turejee kwenye lile suala la kujiuzulu nyadhifa zao kwa waliokuwa vigogo wa Ukawa – Dk. Slaa na Profesa Lipumba. Hakika, kuondoka kwao Ukawa kumeibua tafsiri nyingi na mitazamo mingi kwa Watanzania.

Kuna maswali mengi yanaulizwa mitaani baada ya wiki iliyopita Lipumba naye kuachia ngazi Ukawa. Baadhi ya maswali hayo ni haya: Inakuaje Lowassa akimbiwe kule alikokimbilia? Je, nani wengine ndani ya Chadema, CUF na NCCR wataachia ngazi kwa kusutwa na dhamira zao juu ya suala la kumpokea Lowassa? Je, kuondoka kwa Slaa na Lipumba kumedhoofisha kiasi gani kampeni ya Lowassa ya kuusaka urais kupitia Upinzani?

Kwanza, labda nianze kwa kusema ya kwamba kuondoka kwa Dk. Slaa (Chadema) na baadaye Profesa Lipumba (CUF) kunathibitisha kwamba tangu mwanzo wawili hao hawakupendezwa na hatua ya Ukawa kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea urais wake kupitia Chadema.

Kama hivyo ndivyo, mtu unaweza kujiuliza ni nani hasa walikuwa vinara wa kumkaribisha Lowassa Ukawa na hata kwenye majadiliano ya iwapo aruhusiwe kugombea urais au asiruhusiwe? Hisia za wengi ni kwamba waliokuwa vinara wa kumkaribisha Lowassa Ukawa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia. Dk. Emmanuel Makaidi hatajwi kwa sababu chama chake hakina ushawishi wowote mkubwa nchini japo kimo kwenye Ukawa. Ilivyo hivi sasa, Ukawa imebaki ni ya Mbowe na Mbatia.

Sasa, baada ya Dk. Slaa na Profesa Lipumba kujiondoa, hao wawili (Mbatia na Mbowe) ndio watapaswa wazunguke naye mikoani wakati wa kampeni za urais ili ‘kumsafisha’ dhidi ya tuhuma za ufisadi ambazo zimemwandama kwa miaka 20.

Ikizingatiwa kwamba Mbowe na Mbatia wanatoka Kaskazini (ni Wachaga) ambako pia anatoka mgombea urais Lowassa, utakubaliana nami ya kwamba si watu wanaofaa sana kumpigia kampeni ya urais. Maswali yataulizwa juu ya u-kaskazini wa hao watatu – Mbowe, Mbatia na Lowassa. Hakika, picha ingekuwa tofauti kama angekuwemo Lipumba kwenye kampeni.

Lakini pia lipo suala la Mbowe na Mbatia kugombea ubunge kwenye majimbo yao kule Uchagani. Sioni ni vipi wawili hao wanaweza kuandamana mikoani na Lowassa muda wote wa kampeni ‘kumsafisha’ badala ya kujipigia wenyewe kampeni kwenye majimbo yao Uchagani!

Itapaswa wachague moja - kujipigia kampeni majimboni au kuandamana na Lowassa mikoani kwenye kampeni za urais ili ‘kumsafisha’. Na kama wataamua kubaki majimboni, ni nani wengine ambao hawagombei ubunge wataandamana na Lowassa mikoani ‘kumsafisha!? Au itabidi Lowassa ‘ajisafishe’ mwenyewe wakati wa kampeni?

Nasisitiza tena kwamba hali ingekuwa ni tofauti kama Dk. Slaa na Lipumba wangelikuwa bado ni viongozi wakuu wa Chadema na CUF. Wawili hao wangeliweza kuifanya vyema kazi hiyo si tu kwa sababu wao hawagombei ubunge, lakini pia kwa sababu wanafahamika kote nchini na wana uzoefu wa kampeni za urais kwa kuwa walishawahi kugombea nafasi hiyo.

Ndugu zangu, ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba kujitoa kwa Slaa na sasa Lipumba ni pigo kubwa kwenye kampeni ya urais ya Edward Lowassa kupitia Ukawa. Na hiyo inanifanya nizidi kuamini ya kwamba itakuwa vigumu mno kwa Edward Lowassa kuutwaa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Sote tunajua ya kwamba Lowassa si mzungumzaji mzuri jukwaani na pia afya yake si nzuri sana. Katika hali hiyo, alihitaji sana msaada wa wazungumzaji wazuri kama Profesa Lipumba, Dk. Slaa au Mbowe na Mbatia ambao nimeshasema kuna shaka kama watakuwanaye (Lowassa) muda wote wa kampeni.

Kuna wasomaji wangu walinitumia meseji eti kwamba umaarufu na utajiri wa Lowassa vyenyewe ni kampeni tosha ya kumwingiza Ikulu! Kwamba eti mapesa yake na umaarufu wake vinatosha, na kwamba hahitaji sana kupigiwa kampeni na watu wengine.

Mimi nakataa. Kama mapesa na umaarufu peke yake vinatosha, mbona mwaka 2010 Godbless Lema alishinda ubunge kwa kumbwaga Dk. Matilda Buriani ambaye alisaidiwa na Lowassa kwenye kampeni? Kama mapesa na umaarufu tu vinatosha, mbona hakumwezesha swahiba wake huyo kushinda ubunge?

Lakini pia mbona Lowassa hakufanikiwa kumsaidia mkwewe kumbwaga Joshua Nassari katika uchaguzi ule mdogo wa Arumeru Mashariki licha kwamba yeye (Lowassa) aliamua kujitosa mwenyewe kwenye kampeni kumsaidia mkwewe?

Hapana ndugu zangu, umaarufu na utajiri peke yake havitoshi kumfanya mtu ashinde urais. Yapo mambo mengine mengi ya kuzingatia kama vile uadilifu, weledi, uchapakazi, maono, itikadi nk. Kama mapesa na umaarufu vingekuwa pekee yake vinatosha, basi uchaguzi wa mwaka 2010 Chadema isingeambulia jimbo hata moja mkoani Arusha ambako ndiko ngome kuu ya Lowassa!

Kwa hiyo, wanaoamini ya kuwa Lowassa atashinda urais kwa sababu tu ni maarufu na tajiri wanajidanganya. Wanaoamini ya kwamba utajiri na umaarufu wa Lowassa utawafanya wapiga kura wasahau kabisa tuhuma za ufisadi zinazomwandama kwa miaka 20, watasononeka ukweli utakapojulikana Oktoba mwaka huu.

Hao ni wale wale walioamini au walioaminishwa na kina Mbowe kwamba eti Lowassa akihamia Chadema, basi maelfu ya wanachama wa CCM watamfuata, na hivyo Chadema itashinda kirahisi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Mpaka sasa wiki imeshapita tangu Lowassa ahamie Chadema, na bado hatujayaona hayo maelfu ya wanachama wa CCM wakimfuata! Hali hii inaififisha ile hoja ya umaarufu wake iliyotumiwa na Mbowe na wenzake kumsimamisha agombee urais kupitia Chadema.

Kwa hakika, hata wale waliokuwa maswahiba wake wa karibu katika CCM kama vile Peter Serukamba, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Emmanuel Nchimbi, Adam Kimbisa, Sophia Simba nk mpaka sasa wameamua kubaki huko huko CCM! Mbona hawajamfuata Chadema? Katika hali ya kawaida hao si ndo walipaswa kuwa wa kwanza kutimka naye Chadema kabla hao maelfu wengine hawajamfuata?

Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusisitiza kile nilichokiandika wiki iliyopita; nacho ni kwamba, kwa kuitosa ajenda ya ufisadi ili kumpokea Lowassa, Chadema kimeipoteza nguvu yake kuu ambayo kwayo kilipata umaarufu kilio nao hivi sasa.

Kwa kuwa itakuwa vigumu kwa Chadema kuwaendea wapiga kura mikoani kikiwa na Lowassa na ajenda hiyo ya ufisadi kibindoni, sioni namna yoyote kinavyoweza kushinda uchaguzi wa Oktoba hasa baada ya kuwapoteza Slaa na Lipumba.

Na hapa bado sijaizingatia hoja nyingine kuwa CCM kitaongeza nguvu zake maradufu kuhakikisha Lowassa hatwai dola - iwe ni kwa kuiba kura au mizengwe mingine. Kwa maneno mengine, kama kilipanga mkakati wa ‘bao la mkono’ sasa kinapanga mkakati wa ‘mabao ya mikono’ ili tu kujaribu kuudhihirishia umma kwamba huyo bwana kisiasa hana nguvu na umaarufu huo mkubwa anaohusishwa nao.

Kwa ufupi, lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati kwa Chadema kumpokea Lowassa na kumsimamisha kama mgombea urais wake. Kosa hilo la kina Mbowe limetukatisha tamaa wengi wetu ambao tuliamini kuwa Chadema ni chama bora kinachopinga ufisadi kinachostahili kuwa mbadala wa CCM.

CHANZO: Gazeti la RaiaMwema.

Baada ya jeshi la Polisi nchini Tanzania kupiga marufuku maandamano ya wanasiasa wakati wa kampeni,chama cha wananchi cuf wameibuka na kusema kuwa kauli hiyo ni mzaha wa jeshi la polisi ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwani hakuna sheria inayokataza maandamano ya wanasiasa na hawako tayari kutii sheria hiyo kwani ni uonevu wa watanzania.

Akizungumza na wanahabari mapema asubuhi leo naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho mama MAGDALENA SAKAYA amesema kuwa kuandamana ni haki ya mtanzania ya kikatiba,ambayo imeelezwa kama njia ya kujieleza,hivyo Polisi wanakiuka katiba na sheria za nchi zinazoruhusu kuandamana ambapo pia amesema wanakiuka sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2002 ibara ya 11 ambayo inatambua maandamano na mikusanyiko kama sehemu ya shughuli za kisiasa.

Sakaya anasema kuwa ni kitu ambacho hakiwezi na hakiwezekani wakati wa kampeni kwa vyama vya siasa kufanya kampeni kimya kimya pasipo maandamano ambapo amesema ni utamaduni ambao hata nchi zilizoendelea uliwashinda huku akisema huwezi kutenganisha kuandamana na kampeni kwani ni vitu vinavyokwenda sambamba.

Aidha amesema chama cha wananchi CUF kinaona hizi ni dalili za jeshi la polisi kutumiwa na chama cha mapinduzi CCM ili kuziba aibu wanayoipata kwa kukosa umati wa watu katika mikutano yao.
Mwisho CUF wamesema kuwa hawakubaliani na agizo hilo na kusema kama polisi wataendelea na msimamo huo wao ndio watakuwa wameanzisha vurugu ambazo hazina ulazima katika uchaguzi huo.
Powered by Blogger.