LAZIMA
wakae! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia umati mkubwa kujitokeza
kumsindikiza mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pombe
Magufuli (pichani)kwenda kuchukua fomu ya urais Ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), Posta-Mpya, jijini Dar, Amani linakupa mchapo kamili.
Juzi,
Magufuli (pichani) akiambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu
wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phillip Mangula na Katibu
Mkuu, Abdulrahman Kinana walianza msafara kuanzia kwenye Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu ya CCM, Lumumba kuelekea makao makuu hayo ya NEC kuchukua
fomu hiyo.Wakizungumzia msafara huo uliosimamisha shughuli zote kwa
muda, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar walisema kutokana na muitikio
mkubwa wa wanachama na wasio wanachama waliojitokeza, ni dhahiri
itakapofika siku ya uchaguzi, Oktoba 25, mwaka huu, wapinzani lazima
wakae kwani Magufuli ni jembe.
“Lazima wakae wapinzani, tena na hivi
wanavyoanza kugawanyika mara sijui katibu mkuu wao Slaa amejiengua
hawaiwezi CCM hata kidogo.
“Magufuli
ni msafi, hana doa hata moja. Utendaji wake wa kazi umetukuka. Kila
Mtanzania anajua namna ambavyo amekuwa akisimamia sheria katika ujenzi
wa barabara, kupushi mambo yaende kwenye mstari na hata kuwafokea
hadharani watumishi wanaozembea kazini,” alisema Kery Masabwite mmoja wa
wakazi wa Dar na kuongeza:
“Watu
wengi ambao si wanachama wa CCM wameguswa sana uteuzi wa Magufuli. Kama
hiyo haitoshi, kuna wafuasi wa Chadema na Ukawa ambao hawakufurahishwa
na Edward Lowassa kuingia kwenye chama chao, wote wamekihama na
watapigia kura CCM.”
Wakati
akielekea kuchukua fomu NEC kisha kurejea kuhutubia katika Ofisi Ndogo
za CCM Lumumba kuhutubia, maelfu ya watu waliojitokeza kumsindikiza
walisikika wakimpa jina jipya Magufuli kwa kufupisha jina lake na kuita
JM wakimaanisha John Magufuli ukiachana na yale ya Tingatinga, Jembe na
Burdoza yaliyozoeleka.
Aidha, jina hilo la JM lilikaziwa maana na mnajimu Hassan Yahya Hussein ambaye hivi karibuni alizungumza na Amani
na kueleza kuwa utabiri wake unaonesha kuwa mtu mwenye mvuto wa urais
wa Tanzania lazima kwenye majina yake kuwe na heruf J, M na N.
“Huo
ndiyo ukweli na hata kwa marais waliotangulia, wote majina yao
yameanzia herufi J, M na N. Hivyo hata ajaye lazima jina lake liwe na
herufi hizo,” alisema mnajimu huyo ambapo Magufuli anazo mbili, J na M
(JM).
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara katika ofisi hizo ndogo za CCM mara baada ya
Magufuli kuchukua fomu, Rais Jakaya Kikwete alisema tukio hilo lilikuwa
muhimu kwake hivyo isingekuwa rahisi kutokuwepo.
“Kuchukua
fomu kwa wagombea wetu ni moja ya shughuli muhimu katika chama ndiyo
maana niko hapa leo, najivunia pia juzi kuwepo Australia, walinipongeza
kwa kuongoza kwa demokrasia na kuwapa watu uhuru wa kuchagua chama
wakitakacho. Watanzania wajiandae kwa uzinduzi rasmi wa kampeni
tutakaoufanya Agosti 22, mwaka huu,” alisema Kikwete.
Mbali na Kikwete, shughuli hiyo
ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia wilaya hadi taifa
akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Post a Comment