Kocha
wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameangukia pua kwenye
kura za maoni kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya Udiwani wa kata ya
Kigogo kupitia Chama Cha Mapinduzi baada ya kumaliza akiwa nafasi ya
tatu kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Nimemaliza mtu wa tatu katika kura za maoni kata ya Kigogo
na hiyo siyo maana nimeshindwa kwasababu kawaida ya CCM baada ya kura za
maoni majina yanapelekwa Wilayani na baadae Mkoani ili kupitia jina la
kila mmoja ili kuona yupi anafaaili aweze kwenda lakini kwa jinsi
ambavyo Julio Alberto sikufanya kampeni za kupita nyumba kwa nyumba
kwasababu mimi sera yangu sitaki rushwa”.
Source: Shaffih Dauda
Post a Comment