Natumai
utakuwa u mzima wa afya kabisa. Kama ilivyo matatizo mengine tatizo la
kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa huwakumba na wanaume vilevile ila
siyo kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa wanawake.
Katika makala haya tutaaangalia kwa kina
sababu za tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza
njia za kutatua au kuondokana na tatizo hili.
Mwili wa mwanadamu uliumbwa ukiwa na
matamanio na si mbaya kama mwenye mwili atakuwa na uwezo wa kujitawala.
Wanaume wengi huvutiwa zaidi na hisia za kushiriki tendo kwa kuona
baadhi ya maungo ya wanawake, kusikia sauti na hata migusano.
Kuna wanaume wengi wao wapo tu siku
zinaenda hawapati hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wanajiona kama
ndiyo wamefanikiwa kujitawala kumbe ni wagonjwa.
Habari njema ni kwamba pamoja na tatizo
hili kuwasumbua watu wengi kuna mambo unayoweza kuyafanya
kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa, kwa kutumia mimea
tiba na matunda tiba.
Unachotakiwa kufanya kama umejaribu
kutumia njia mbalimbali ili kuondoa tatizo hili bila mafanikio basi wahi
mapema kwa wataalamu ufanyiwe uchunguzi au ukatutembelea Sigwa Herbal
Clinic tukakusaidia kuliondoa kabisa tatizo hilo na ukarejea katika hali
ya kawaida. Baadhi ya watu wanaamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa
inapungua kadiri umri wa mwanaume unavyoongezeka. Kuna idadi kubwa tu
ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata
umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa
tatizo hili.
Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake.
Hata hivyo, tatizo la mwanaume kukosa
hamu ya kushiriki tendo limekuwa ni chanzo kikubwa katika kuleta
migogoro katika ndoa nyingi.
Wanaume kwa kawaida ni wabishi sana na
huwa hawapendi kuaibika hivyo mtu anaweza akawa na tatizo ila hapendi
mwenzi wake ajue kama ana tatizo ambalo kumbe angeliweka bayana angepata
ushauri wa namna ya kulitatua.
Pamoja na kwamba tatizo hili
halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa
kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, ni sawa na uwiano
wa mwanamme mmoja mwenye tatizo hili katika kila wanaume sita au saba.
Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume.
Tatizo hili huwakera zaidi wanaume
kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya
ukamilifu wa mwanamme na hukosa raha wanapoona wana mapungufu kuhusu
mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.
Natumai utakuwa u mzima wa afya kabisa.
Wiki iliyo pita tulianza kuaangalia sababu zinazopelekea wanaume kukosa
hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenza wake.Kama nilivyoeleza wiki
iliyopita ni kwamba; katika Makala haya tutaaangalia kwa kina sababu za
tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza njia za
kutatua au kuondokana na tatizo hili.
Leo tutaangalia sababu au vyanzo vinavyopelekea mwanaume kukumbwa na tatizo hili la kukosa hamu ya kushiri tendo la ndoa.
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume linaweza kusababishwa na vitu vingi sana.
Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile
au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu
tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.
Mahusiano Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke
Uhusiano kati ya mwanume na mwanamke ambao ni wanandoa una mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa matamanio ya mwanaume.
Kama kutakuwa na matatizo ya mahusiano
kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha
tatizo la kukosa hamu ya mapenzi.
Ni vema ukajihoji kama mahusiano yako na
mwenza wako yapo sawa. Na mara nyingine unaweza ukawa umekuwa katika
mahusiano kwa mda mrefu kiasi ambacho umemzoea hali inayopelekea kukosa
hamu ya kushiriki nae tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji
wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu
ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja
na;Madawa ya high blood pressure, Madawa ya kuondoa msongo wa mawazo,
Madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa
mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone.
Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni
inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo
la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili.
Kama thyroid haitoi homoni za kutosha,
tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili
ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika
eneo la shingo.
Umri Kuwa Mkubwa
Kiwango cha testosterone katika mwili wa
mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anvyozidi
kuwa na umri mkubwa. Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya
mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanaume homoni hii hutolewa kwa
kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari.
Homoni ikipungua katika mwili wa
binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha
testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanaume huyu humfanya asiwe
na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze
hamu ya kufanya mapenzi.
Natumai utakuwa u mzima wa afya kabisa.
Wiki iliyo pita tulianza kuaangalia sababu zinazopelekea mwanaume kukosa
hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenza wake. Kama nilivyoeleza wiki
iliyopita ni kwamba; katika Makala haya tutaaangalia kwa kina sababu za
tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza njia za
kutatua au kuondokana na tatizo hili.
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo
la ndoa kwa mwanaume linaweza kusababishwa na vitu vingi sana.
Nikukumbushe tu kwamba sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au
kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Fuatilia kwa
makini;
Uchovu.
Wakati mwingine uchovu hupelekea mtu
kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Na ikiwa mtu atakuwa anasongwa
na shughuli nyingi zinazochosha mwili kiendelevu hamu ya kushiriki tendo
la ndoa huanza kupungua na ikizidi basi baadaye mwanaume husika atakosa
hamu ya kushiriki tendon la ndoa na itahitaji uangalizi mkubwa ili
arejee katika hali yake ya kawaida. Vilevile kukosa mpango mzuri wa
shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya
mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi
yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.
MsongoWa Mawazo
Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya
kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha hali
inayopelekea kushindwa kuyafanya mambo yako ya kawaida kiufanisi.
Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na
matamanio yako ya kimapenzi. Mwanaume anasongwa na mawazo kiasi cha
kuathiri katika ufanisi wa shughuli zake anaweza kupoteza hamu ya
kushiriki tendo la ndoa.
Kuwahi kufika kileleni
Katika vitu ambavyo wanaume wengi
hawapendi vijulikane na wenzi wao ni tatizo la kuwahi kufika kileleni.
Kila mwanume hupenda aonekane ni rijali au mwanaume kamili mwenye uwezo
wa kushiriki tendo la ndoa bila shida yoyote. Na imezoeleka katika jamii
zetu ikiwa mwaume atakuwa ana tatizo la kuwahi kufika kileleni anaweza
akatangazwa mtaa mzima kila mtu ajue, hali hii hupelekea aibu kubwa na
fedheha.
Katika mazingira kama hayo mwanume
mwenye tatizo hilo hata kama hajatangazwa na mwenzi wake amemtunzia siri
hiyo, anajihisi kuwa hafai. Hali hii humfanya kila anapopata hamu ya
kushiriki tendo la ndoa aogope kushiriki tendon a mwenza wake kwani
ataabika. Hii inamchango mkubwa sana katika kumfanya mwanume apoteze
hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Tumekuwa tukiangalia tatizo la wanaume
wengi kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Tumeangalia jinsi tatizo hili
linavyoisumbua jamii yetu na pia tumejua kuwa mwanaume kukosa hamu ya
kushiriki tendo la ndoa si jambo la kawaida ni tatizo linaloweza
kutibika. Zifuatazo ni njia za kuondoa tatizo la kukosa hamu ya
kufanya tendo la ndoa
Wengi wanatarajia kuambiwa wameze dawa
fulani ili kuondokana na tatizo hilo. Kama unatatizo hilo ni vema
ukawaona matabibu kwa ushauri na uchunguzi ili kujua chanzo cha tatizo
na upate matibabu. Ni vema kwa wanaume wenye tatizo hilo washirikiane na
wake zao ili kuliondoa tatizo hilo.
Katika nchi zilizoendelea, wataalam
wamekuwa wakigundua dawa na vifaa tiba vipya vya kuondoa tatizo hili
na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo
ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction
Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs. Habari njema ni kwamba
tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa mimea tiba na matunda tiba ya
kawaida ambayo ipo katika mazingira yetu yanayotuzunguka.
Utafiti umeonyesha kuwa tunachokula
ndicho kinachotujenga na kutufanya tuwe watu wa aina gani. Vyakula
tunavyokula vina mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa afya zetu
hivyo nimuhimu kuwa makini katika kuamua tule nini na tunywe nini. Kuna
uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi.
Baadhi ya chakula na virutubisho vimehusishwa na hamu ya kushiriki
tendo la ndoa.
Virutubisho ndani ya chakula ambavyo
vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na
zinc. Kirutubisho cha zinc kinaongeza mbegu kwa mwanamme (sperm count)
hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chakula cho
chote chenye virutubisho hivi vikiliwa humfanya mlaji asikie hamu ya
kushiriki tendo la ndoa.
Baadhi ya vyakula kula na matunda tiba hayo ni kama vile:
Tikitimaji-Hili linachukuliwa kuwa ndilo
tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia
92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline
ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya
mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita
vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri
zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia
za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha
mwanamke na ndani ya uume wa mwanamme.
Parachichi -Tunda hili lina vitamini E
ambayo ni antioxidant. Ndani ya tunda hili kuna potassium na vitamini B6
ambavyo huboresha afya ya moyo na kusaidia mzunguko wa damu.
Strawberries–Tunda hililina antioxidants
kwa kusaidia afya ya moyo na mishipa ya damu (arteri) na vitamin C
ambayo huongeza kiwango cha mbegu kwa mwanaume.
Kuna mchanganyiko wa matunda ukisagwa
pamoja na kunywewa umeonyesha kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Kwa ziada unaweza kutumia karafuu, mayai na tangawizi pia.
Nakushauri msomaji wangu ufuatilie kwa
makini Makala haya ili kujua vizuri kuhusu tatizo hili. Lakini kama una
tatizo hili na unajisikia aibu kumweleza mwenzi wako tupigie simu katika
namba zetu au tutembelee Sigwa herbal Clinic katika vituo vyetu
vilivyopo Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga, Kigoma,
Mwanza.
Nakushauri msomaji wangu ufuatilie kwa
makini Makala haya ili kujua vizuri kuhusu tatizo hili. Lakini kama una
tatizo hili na unajisikia aibu kumweleza mwenzi wako tupigie simu katika
namba zetu au tutembelee Sigwa herbal Clinic katika vituo vyetu
vilivyopo Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga, Kigoma,
Mwanza.
Post a Comment