MUNGU akimjalia uhai msanii Bambo, msimu ujao wa uchaguzi mkuu
atajitosa miguu yote kuwania udiwani lakini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA).
Hiyo ni baada ya siku chache zilizopita kujiondoa kwenye
kinyang’anyiro hicho cha udiwani wa Kata ya Mchikichini, Ilala alipokuwa
anagombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Saluti5 wiki hii, Bambo alisema kuwa, tofauti na mwaka
huu, anaamini msimu ujao atakuwa amejipanga kikamilifu pamoja na fursa nzuri ya
kuhimili mikiki ya uchaguzi.
Hata hivyo, Bambo hakuweza kuweka wazi sababu inayomfanya aitose CCM
na kuhamia CHADEMA katika msimu huo ujao wa kinyang’anyiro cha uchaguzi
Post a Comment