Katibu
wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku,akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo kwenye picha) juu ya chama hicho kuhamwa na Mwenyekiti wake wa
mkoa, Mgana Izumbe Msindai aliyehamia CHADEMA.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
KURA
za maoni nafasi ya udiwani,ubunge wa viti maalum na ule wa majimbo
CCM mkoani Singida, zimeacha malalamiko na maumivu mengi,ambayo ni
pamoja na kuhamwa na wananchama wake wengi akiwemo Mwenyekiti wake wa
mkoa, Mgana Izumbe Msindai na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ikungi
Christina Samwel Hamisi,kujivua uanachama na kujifukuzisha kwenye nafasi
zao za uenyeviti,kwa tuhuma ya kukiuka sheria, taratibu na kanuni.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana,katibu wa CCM mkoa wa
Singida,Mary Maziku, alisema Msindai kiongozi wao huyo wa muda mrefu
ndani ya chama,hajamjulisha azma yake ya kukihama chama, isipokuwa
aliwasiliana na Katibu Msaidizi kuwa mali yake binafsi itolewe kwenye
ofisi yake ya CCM.
Alisema
CCM mkoa wa Singida kuhamwa na mwenyekiti wake, hakitaterereka hata
kidogo na zaidi kitaendelea kusonga mbele ikiwemo kuhakikisha majimbo
yote kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu,yanakuwa mikononi mwa CCM.
“Mimi
niseme tu kuwa namwombea kila la kheri aliyekuwa Mwenyeiti CCM mkoa na
bosi wangu,kwenye safari yake ya kusaka mafanikio makubwa zaidi ambayo
ameyakosa ndani ya CCM”,alisema Maziku.
Ingawa
haijafahamika hadi sasa, ni nini kimemsibu hadi ahame CCM mahali ambako
alipewa cheo kikubwa cha mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa yote
nchini,inadaiwa ni kutokana na kushindwa kwenye kura za maoni ubunge
jimbo la Mkalama,hivi karibuni.
Kwenye
kura hizo za maoni,Msindai alikuwa mshindi wa pili kwa kupata kura
3,908 dhidi ya mshindi Allan Joseph Kiula,aliyepata kura 5,823.
Kwa
upande wa Mwenyekiti UWT wilaya ya Ikungi,Chrisita,baada ya kushindwa
kwenye kura za maoini ubunge viti maalum,siku nne baadaye,alihamia
CHADEMA ambapo alichukua fomu kuomba ubunge viti maalum kupitia chama
hicho cha upinzani,aliishia kupata kura sifuri (0).
Kwa
mujibu wa Katibu Maziku,mwanachama au kiongozi anapohama CCM na
kujiunga na chama kingine cha upinzani,automatiki atakuwa amejivua
uanachama na nyadhifa zote za uongozi endapo alikuwa nazo.
Katika
hatua nyingine, Mwigulu Nchemba, ametetea kwa kishindo nafasi yake ya
ubunge wa jimbo la Iramba magharibi kwa kupata kura 25,786 na mpinzani
wake David Jairo,akuambulia kura 1,975,Juma Hasan Kilimba (1,827) na
Amon Gyuda (236).
Kwa
jimbo la Singida mjini liloachwa wazi na Mohammed Gulam Dewji, Maziku
alisema kilichotendeka kwenye uchaguzi wa nafasi ya ubunge, imelazimu
matokeo yake yatatolewa na katibu mkuu CCM Abrahaman Kinana huko Dodoma
siku ambayo hadi sasa haijafahamika.
Elibariki
Emmanuel Kingu,mkuu wa wilaya ya Igunga ameshinda nafasi ya ubunge
jimbo la Singida magharibi kwa kupata kura 4,759.Kingu amewahi kuwa mkuu
wa wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora.
Wengine
na kura zao kwenye mabano,kuwa ni Dinawi Samwel Gabriel (901),Hamisi
Shaban Lissu (1,918),Willson Elisha Nkhambaku (2,836),Dk.Hamisi Hema
Mahuna (1,013),Dk.Grace Khwaya Puja (762),Yona Daud Makala (252) na
Hamisi Hassan Ngila (384).
Kwa
upande wa jimbo la Ikungi mashariki,katibu huyo alisema Jonathan Andrew
Njau ameshinda kwa kupata kura 6,312 na kufuatiwa kwa mbali na Mdimi
Emmanuel Hongoa aliyepata kura 1,564.
Wengine
na kura zao kwenye mabano kuwa ni Hamisi Abeil Maulid (1,409),Jacob
Theophil Kituu (515),Emmanuel Japhaet Hume (454) na Martin Labia Lissu
(1,291).
Katibu
wa CCM wilaya ya Manyoni,Dafroza Lucas,alisema nafasi ya ubunge jimbo
la Manyoni magharibi,limechukuliwa na mwenyekiti wazazi wilaya ya
Manyoni,Yahaya Omari Masare aliyepata kura 6,164 na kufuatiwa na mbunge
aliyemaliza muda wake,John Paulo Lwanji,aliyepata kura 2,651.
Dafroza
alitaja wagombea wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Elphas
Eammanuel Lwanji (1,387), Jamal Juma Kuwingwa (403),Jane Lucas Likuda
(396) Mojammed Juma Makwaya (280),Yohana Stephen Msita (482),Moshi Musa
Mmanywa (508),Adimini Mwakapalila (Msokwa (985),Dk.Mwanga Mkayangwa
(1,745),Rashid Ramadhani Said (199) na Francis Pius Shaban (80).
Jimbo
la Manyoni mashariki,alisema nafasi ya ubunge imechukuliwa na Daniel
Edward Mtuka (6,792) akifiatiwa kwa karibu na Dk.Pius Stephen Chaya
(6,270).
Dafroza
alitaja wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni,Gaitani Francis
Romwald (1,542),Joseph Meshack Chitinka (592),AlexNyamejo Manonga
(433),Jumanne Bosco Mtemi (715) ,Eng.Horold Jackson Huzi Mtyona (1,212)
na Gaitaini Francis Romwald (1,542)
Post a Comment