Baada ya jeshi la Polisi nchini Tanzania kupiga marufuku maandamano ya wanasiasa wakati wa
kampeni,chama cha wananchi cuf wameibuka na kusema kuwa kauli hiyo ni mzaha wa
jeshi la polisi ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwani hakuna sheria
inayokataza maandamano ya wanasiasa na hawako tayari kutii sheria hiyo kwani ni
uonevu wa watanzania.
Akizungumza
na
wanahabari mapema asubuhi leo naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho mama
MAGDALENA
SAKAYA amesema kuwa kuandamana ni haki ya mtanzania ya kikatiba,ambayo
imeelezwa kama njia ya kujieleza,hivyo Polisi wanakiuka katiba na sheria
za nchi zinazoruhusu kuandamana ambapo pia amesema wanakiuka sheria ya
vyama vya
siasa ya mwaka 2002 ibara ya 11 ambayo inatambua maandamano na
mikusanyiko kama
sehemu ya shughuli za kisiasa.
Sakaya anasema kuwa ni
kitu ambacho hakiwezi na hakiwezekani wakati wa kampeni kwa vyama vya siasa
kufanya kampeni kimya kimya pasipo maandamano ambapo amesema ni utamaduni ambao
hata nchi zilizoendelea uliwashinda huku akisema huwezi kutenganisha kuandamana
na kampeni kwani ni vitu vinavyokwenda sambamba.
Aidha amesema chama cha
wananchi CUF kinaona hizi ni dalili za jeshi la polisi kutumiwa na chama cha
mapinduzi CCM ili kuziba aibu wanayoipata kwa kukosa umati wa watu katika
mikutano yao.
Mwisho CUF wamesema
kuwa hawakubaliani na agizo hilo na kusema kama polisi wataendelea na msimamo
huo wao ndio watakuwa wameanzisha vurugu ambazo hazina ulazima katika uchaguzi
huo.
|
Post a Comment