Aah! Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alijikuta akipigwa butwaa kufuatia kitendo cha mcheza shoo wake, Moses Iyobo Ă«MozeĂ­ na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel kuoneshana ‘mahaba nipeleke kuzimu’ hadharani.

Tukio hilo la Diamond kupagawishwa na mahaba ya wawili hao lilijiri usiku wa kuamkia Agosti 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Iyobo. Lakini kabla ya kufika kwenye tukio hilo, twende hatua kwa hatua.

MWONEKANO WA DIAMOND UKUMBINI

Akiwa kwenye sherehe hiyo iliyojazwa pia na mastaa, muda mwingi Diamond alionekana mwenye furaha ya hali ya juu kufuatia mishemishe za bethidei hiyo iliyoandaliwa na Aunt kama moja ya kumshtukiza ‘sapraizi’ mpenzi wake huyo.

Habari zinasema mpaka Iyobo anaingia ukumbini hapo alikuwa hafahamu kama kuna sherehe ya kuzaliwa kwake.

 
MUDA WA MSHTUKO

Iyobo alizama ukumbini hapo saa 7 usiku kwa kuitwa na Aunt. Aunt pia ni staa wa sinema za Kibongo.

Baada ya Iyobo kuingia ukumbini alipata mshtuko kufuatia Diamond na nyota wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kumkaribisha kwa kummwagia maji na vinywaji mbalimbali ambapo waalikwa wengine nao waliungana kumuogesha huku wakimwimbia ‘hepi bethidei tu yu.’

DIAMOND AFUNGUA SHAMPENI

Baada ya zoezi la kumkaribisha Iyobo aliyekuwa amelala zake nyumbani kwa Aunt kumalizika, Diamond alipewa chupa ya kinywaji aina ya shampeni kwa ajili ya kufungulia sherehe hiyo ambayo ilianza hapo.

DIAMOND ACHEZA HUKU NA KULE

Katika hatua nyingine, waalikwa walitumbua macho kumwangalia Diamond ambaye muda mwingi alikuwa akicheza tena kwa vituko mbalimbali.

ABEBA KEKI

Pengine ni kwa sababu ilikuwa bethidei ya mcheza shoo wake, kwani ulipofika wakati wa kupeleka keki mezani, Diamond aliibeba yeye hadi eneo husika kwa ajili ya ‘kulishania’.

MAHABA NIPELEKE KUZIMU SASA!

Sasa wakati Aunt na Iyobo wakiwa katika tukio la kulishana keki kwa mtindo wa mahaba nipeleke kuzimu (mdomo kwa mdomo), Diamond alionekana kushtuka na kuwatumbulia macho (angalia picha ukurasa wa mbele).

Diamond aliendelea kuwatumbulia macho kama anayewachungulia huku akipanua mdomo kwa mshangao ambapo wawili hao wala kiroho hakikuwadunda kwamba wapo laivu.

KUMBE IYOBO ALIFUNDISHWA

Baada ya kuwashangaa wawili hao kwa karibia sekunde kadhaa, Diamond aliibuka na kusema kuwa, kulishana keki wawili hao kwa staili hiyo, ndivyo WCB ilivyomfundisha Iyobo kwamba, anapokuwa na mpenzi wake huyo sharti amlishe kwa kinywa na si kutumia uma.

DIAMOND HAWEZI KUFANYA HIVI KWINGINE

Jambo ambalo lilijitokeza kwenye sherehe hiyo ambapo waalikwa walisema katu, Diamond hawezi kulifanya hivyo kwenye sherehe nyingine (mbali na jukwaani) ni kitendo chake cha kuimba zaidi ya nyimbo zake tano ukiwemo Nana unaotamba kwa sasa. Huwa akialikwa mahali, Diamond huimba wimbo mmoja au mbili tu.

Hata hivyo, Diamond mwenyewe alisema kuimba nyimbo zote hizo na kuruhusu waalikwa kucheza ni moja ya kuonesha upendo na hamasa yake kwa Iyobo kwani bila yeye hakuna Diamond wala WCB kwa jumla.

USIRI WA UMRI KAMA KAWAIDA

Hata hivyo, kama kawaida, mpaka mwisho wa shughuli hiyo, haikuelezwa wazi kwamba, Iyobo alikuwa akisherehekea kutimiza miaka mingapi ya kuzaliwa kwake zaidi ya kusemwa; ametimiza miaka kadhaa!

Post a Comment

Powered by Blogger.