Kocha
wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameangukia pua kwenye
kura za maoni kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya Udiwani wa kata ya
Kigogo kupitia Chama Cha Mapinduzi baada ya kumaliza akiwa nafasi ya
tatu kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Nimemaliza mtu wa tatu katika kura za maoni kata ya Kigogo
na hiyo siyo maana nimeshindwa kwasababu kawaida ya CCM baada ya kura za
maoni majina yanapelekwa Wilayani na baadae Mkoani ili kupitia jina la
kila mmoja ili kuona yupi anafaaili aweze kwenda lakini kwa jinsi
ambavyo Julio Alberto sikufanya kampeni za kupita nyumba kwa nyumba
kwasababu mimi sera yangu sitaki rushwa”.
Wanamichezo
wengine walioangukia pua kwenye kura za maoni ni pamoja na Afisa habari
wa Yanga Jerry Muro na Abdalla Idirisa Majura waliokuwa wakiwania
kuteuliwa na chama chao kuwania Ubunge wa jimbo la Kawe.
Source: Shaffih Dauda
Post a Comment