Wakati
vyama vinne vinavyounda UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea
urais, vyama vingine vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga
mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa SAU, Ali
Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo
kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa
sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na
mchango katika harakati hizo.
Mwenyekiti wa
APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini mabadiliko
kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono UKAWA.
“Uchaguzi wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,000, lakini pia tuna madiwani watatu na wanachama wameongezeka kwa hivyo ninaamini mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa UKAWA,”
Mwenyekiti
wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema chama hicho
kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea mmoja kutoka CCM au UKAWA.
“Nafasi ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati ya vyama hivyo wakati wa kampeni.”
Post a Comment