Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim
Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kina wagombea wawili
wanaowania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Madai hayo mapya ya Profesa Lipumba yametolewa siku tatu baada ya
kujiuzulu uenyekiti CUF, akisema hiyo ni moja ya sababu za kuachia
nafasi yake kutokana na uamuzi uliofikiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuhusu mgombea urais.
Akizungumza wakati akitangaza kujiuzulu wiki iliyopita, Profesa Lipumba
alisema dhamira yake ilikuwa inamsuta kwa kuwaingiza ndani ya Ukawa watu
kutoka CCM, waliokuwa wanapingana na maoni ya wananchi kuhusu rasimu ya
Katiba ya Jaji Warioba na kuwapa fursa ya kuwania urais.
Post a Comment