Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano CCM Makao Makuu Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaam ambapo alizungumzia ratiba ya vikao vya chama vitakavyoanza mjini Dodoma kuanzia tarehe 8 mpaka 9 Agosti, Kamati Kuu tarehe 10 mpaka 11 Agosti na Halmashauri Kuu tarehe 12 mpaka tarehe 13 Agosti 2015.
 Pia Mgombea mteule wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. John Magufuli, kesho Jumanne, Agosti 4, 2015, atatinga Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.


Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshi la Polisi.


Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM, atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk.Magufuli alichaguliwa na Mkutnao Mku wa CCM, uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose

Post a Comment

Powered by Blogger.