Toka July 28 2015 siku ambayo Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Edward Ngoyai Lowassa alitambulishwa kujiunga CHADEMA na kukabidhiwa Kadi ya Chama hicho, zikaanza kuandikwa headlines Magazetini baada ya kutoonekana kwa Dk. Slaa katika Vikao mbalimbali vya Chama hicho.

Mbowe II

Haya ndio majibu ya Freeman Mbowe kuhusu ishu ya kutoonekana kwa Dk. Slaa >>> “Dk. Slaa ni Kiongozi ambaye wote tunamheshimu, tunampenda na tutaendelea kumpenda siku zote kwa sababu Chama hiki ni cha kujengana na sio kubomoana… Kamati Kuu ya Chama ilifanya Vikao kutafakari ujio ambao tumeupata, tulifanya mashauriano ya muda mrefu halikuwa jambo jepesi na tukaridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Mheshimiwa Lowassa na wenzake ni mpango wa MUNGU ambao tunatakiwa kuunga mkono utusaidie kuwaunganisha wenzetu wa NCCR, CUF na Watanzania wote ili tufikie malengo ya pamoja

Katika hatua zote tulikuwa sambamba na Dk. Slaa, katika dakika za mwisho Dk. Slaa akatofautiana kidogo na Kamati Kuu, tulizungumza nae hata jana nimekuwa na Kikao na Dk. Slaa kwa masaa mawili


Kwenye sentensi nyingine Freeman Mbowe ameongea na haya >>> “Uchaguzi uko karibu, tukakubaliana na Dk. Kwamba sisi tuendelee akiwa tayari tutaungana mbele ya safari tutaendelea kufanya kazi pamoja… Tumemkubalia Dk. Slaa mapumziko ili tujiandae kwenda kwenye Uchaguzi, hatuna ugomvi… achaneni na mitandao inachoandika, ni mambo ya kizushi, hatuwezi kuzuia safari ya Mamilioni kwa sababu ya matakwa ya Mbowe au ya Slaa“–

Nilisema jambo hili nitaliongea mbele ya waandishi wa Habari bila kificho, kama kuhukumiwa nihukumiwe kwa sababu wajibu wangu kama Kiongozi ni kuwa mkweli

Tumekubaliana apumzike kwa muda, tunamwombea MUNGU amtie nguvu na ampe ujasiri wa kuona kauli ya wengi ni kauli ya MUNGU… Nafasi yake kwenye Chama ipo, nafasi zetu za uongozi ni dhamana… Tuwe na amani, Chama chenu kiko salama sana” >>>> Freeman Mbowe.

Alichokisema Freeman Mbowe kiko kwenye hii video pia.


Post a Comment

Powered by Blogger.