Ni napenda kuungana na watanzania wote hususani wanachama wa vyama vinavyounda 
UKAWA ambao wengi wao wamestushwa, kukerwa na kushangazwa na kile 
kilichofanywa na viongozi wa UKAWA ambacho kimeonyesha wazi kuwa umoja huo 
hauna uzalendo KWA Taifa bali viongozi waliopo katika umoja huo wamejawa uchu 
wa madaraka na ubinafsi uliokithiri. Ni nani asiyejua ndani ya Nchi hii uchafu 

ulioanikwa na viongozi hawa hawa wa Ukawa juu ya edward Lowassa? Hali hii 

imenifanya naamini kuwa kwa sasa siasa imevamiwa na maharamia.

LAKINI NINI KINAMSUKUMA LOWASSA KUSAKA URAIS HATA KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA?

KATIKA uhalisia ni wazi kuwa Lowassa ametumia pesa nyingi KATIKA mchakato wa 

Uchaguzi kuliko hata gharama ya kuendeshea TUME ya Uchaguzi. Je pesa hii 

aliitoa wapi?
Duru za uhakika zinasema pesa hiyo ilichangwa na wa fanya biashara wakubwa 

nchini, makampuni makubwa nje ya Nchi, na Nchi za kigeni zenye uchu wa kuunda 

mikataba ya kuchuma raslimali mbalimbali humu nchini. Makubaliano ya kutolewa 

pesa hiyo ni kwamba Lowassa atakapo fanikiwa kushinda watu hao watapewa fursa 

za uwekezaji na makampuni kadhaa yatasamehewa kodi huku Nchi kadhaa zikiahidi 

kutoa misaada mdogo mdogo KWA wananchi kwa tenda za "Dili" za Serikali. Hali 

hii ni hatari sana kwa wananchi wa hali ya chini.
KWANINI LOWASSA KAHAMIA CHADEMA?
Kuhamia kwa Lowassa CHADEMA tunaweza kusema ni haki yake kikatiba lakini 

uhalisia ni kwamba Shinikizo kutoka kwa watu waliowekeza kwa Mgombea huyu KWA 

kutoa mabilioni ya fedha ndio kunamfanya agombee kwani wafadhiri wa harakati 

hizo wamegoma kumuelewa kabisaa Lowassa kwani aliwahakikishia kuwa lazima 

atapitishwa na CCM hivyo kuwa fanya wamwage pesa wakijua wazi wanapalilia 

"deal".

Baada y kukatwa kwa Lowassa ndani ya CCM wawekezaji hawa KATIKA siasa 

walishinikiza kurejeshewa pesa zao lakini Mzee Lowassa asingeweza kuwa 

rejeshea pesa hiyo. Kilichofuata yalikua mazungumzo kati ya Lowassa na CCM 

akiwaomba basi wamsaidie kulipa mabilioni hayo ya Pesa lakini Chama cha 

Mapinduzi kilisema KWA msimamo kuwa hakitolipa Pesa hiyo na hakuna sababu ya 

kulipa Pesa isiyo na manufaa kwa watanzania. Sasa hali ilikua ngumu baada ya 

baadhi ya wafadhiri kuamua kumfirisi Lowassa au kumtaka ajitose KWA gharama 

yoyote kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais kupitia upinzani. Hii INA maana 

Lowassa ameingia upinzani kwa shinikizo la Wafadhiri wake ili kutetea maslahi 

ya Wafadhiri hao.

Hapo nadhani watanzania tuwe wazalendo kwa Taifa, pingeni kwa uwazi ujio wa 

Fisadi LOWASSA katika kivuli cha UKAWA. Ninawapongeza wana Ukawa wanaozidi 

kustukia mchezo kila dakika iendayo kwa Mungu. Tuungane kutetea raslimali 

mbalimbali za Nchi Yetu, tusikubali kuuza Nchi Yetu.

Josias Charles @2015

Post a Comment

  1. Mwandishi unashangaza kwa hitimisho lako. Nchi ilishauzwa na CCM.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.