Tangu
chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA kibadilishe njia yake ya
kuusaka uongozi wa Taifa hili kwa kumsajili waziri mkuu mstaafu Edward
lowasa kumekuwa na story mfululizo zilizokuwa zinaeleza kuwa kuna baadhi
ya viongozi wa chama hicho wamesusa kushiriki katika vikao vya chama
hicho kutokana na kutokubaliana na uteuzi wa mh LOWASA. Viongozi waliokuwa wanatajwa ni pamoja na mwasheria wa chama hicho Mh TUNDU LISSU,na Naibu katibu mkuu Bara mh JOHN MNYIKA ambao kwa pamoja walihusishwa katika sakata hilo. Leo inaweza kuwa ni mwisho wa story hizo baada ya viongozi hao kuonekana katika mkutano mkuu wa baraza kuu la chama hicho KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA tofauti na wengi walivyodhani kuwa hawatashiriki katika vikao tena. Mh mnyika akizngumza na mwandishi wa mtanzao huu amesema kuwa sababu pekee iliyomfanya asionekane kwa kipindi kirefu tokea usajili wa LOWASA ufanyika ni matatizo ya kiafya na sasa yupo fiti kukitumikia chama hicho. |
Post a Comment