Mwenyekiti wa Chdema Taifa, Freeman Mbowe akihutubia  wajumbe wa Baraza Kuu katika ukumbi wa mikutano wa LAPF, Makumbusho jijini Dar mchana huu.
Mbowe-Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sis tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.

Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.

Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.

Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.

Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.

Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko 

Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho

Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi

Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua

Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM. 

Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.
1
2
3
4
5
6Wajumbe wa Baraza Kuu wakifuatilia mkutano huo.
Kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaendelea hivi sasa katika ukumbi wa mikutano wa LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema chama hicho hakiendeshwi kwa siri, kinaendeshwa kwa mikakati

Post a Comment

Powered by Blogger.